Kwa wote waliohitimu Kiswahili IV ama madarasa ya Mazungumzo ya Kiswahili, Fasihi ya Kiswahili au yote matatu na wasiotaka kusahau Kiswahili chao. Tangu mwaka 2008 tunashirikiana na Taasisi ya Mashariki ya Kisasa (ZMO) tukikutana mara moja kwa mwezi kwa kikao cha 'Baraza la Kiswahili' ili tujadili masuala anuwai ya utafiti wa taaluma yoyote ihusuyo Kiswahili. Katika vikao vya kawaida tunatarajia kushughulikia filamu mbalimbali za kisasa za Kiswahili. Nchini Tanzania siku hizi tasnia ya filamu imekua sana. Kila juma filamu mpya tano au zaidi za 'Bongowood' huzinduliwa. Sisi tutachagua filamu tatu nne tukazitazame na kuzijadili pamoja. Kila mwanafunzi atatakiwa kutayarisha sehemu mojawapo ya filamu, yaani maudhui, lugha yake, utengenezaji wake na sifa zake za kimtindo kwa jumla. Lugha itakayotumika darasani ni Kiswahili kitupu. Marejeo ya filamu yatatolewa mwanzoni mwa darasa. |